Monday 29 April 2013

MUME WANGU HANA PUMZI KITANDANI....KWAKE DAKIKA TATU NI NYINGI SANA....NAOMBENI USHAURI

Mimi ni mdada wa miaka 27 na nina watoto wawili kwa sasa nimeolewa na mkaka mwenye miaka 32.

Kwa kweli mume wangu ni kijana handsome. Katika maisha yangu ya usichana mpaka kuolewa nimekuwa na mahusiano na wanaume takribani 4 kabla ya mume wangu.

Wanaume hao wote kwakweli walikuwa nao wazuri  na kati yao wawili walikuwa waume za watu na walikuwa na maumbile yakunitosha.... 



Pamoja na maumbile  yao,sikuwahi kufika kileleni japokuwa walikuwa wanapumzi ndefu yaani walikuwa wanaweza kuplay for about  1 hour . Tena kama tutalala pamoja usiku huo walikuwa wanaweza hata 4-5.

Nilipompata mume wangu nilimpenda toka rohoni na baada ya mhusiano ya miaka miwili tulioana,tatizo ambalo lipo kwenye ndoa yangu na nililiona toka mwanzo ni kwamba mume wangu hana pumzi kitandani japokuwa ndio mwanaume pekee anayenifikisha kileleni .

 Yaani mume wangu yeye ni 3 minutes tu amemaliza  na baada ya muda anakoroma, hatuwezi kufanya hata mara  mbili kwa usiku hata nikimchezea anashindwa kusimama labda afanye kimoja asubuhi kingine usiku.

Na ili nikojoe kuna staili lazima niziapply mimi mwenyewe niwe najigusa kwake maana yeye tukifanya anashindwa kujizuia mara moja anakojoa.

Nisaidieni wapendwa nifanyaje maana  bado  nampenda  mume  wangu."
---------------


Jibu la Dyna: 

Shukurani sana kwa ushirikiano, hongera kwa kufanikiwa kufika kileleni kwani sio wanawake wote hufika hapo. Sidhani kuwa ni kweli kuwa mumeo anakojoa ndani ya dakika 3 na wakati huohuo wewe unafika kileleni.

Unapokuwa kwenye uhusiano wa kudumu au ndoa hupaswi kabisa-kabisa kurudisha mawazo yako nyuma na kuanza kufananisha utendaji wa wanaume uliokuwa nao na mpenzi wako wa sasa/mumeo. Jifunze kukubali jinsi mumeo alivyo na ridhika n
a uwezo wake aliojaaliwa na Mungu.

Ndio maana kabla ya uchumba kutangazwa kule kwetu huwa kuna swali unaulizwa na mama au bibi au shangazi


- "je una uhakika kuwa unataka kuolewa na huyu bwana? 


-je uko radhi kuishi nae hata kama siku moja utagundua kasoro zake? (kasoro hapa wanamaanisha kushindwa kufanya tendo). 


Hivyo basi unapofunga ndao na mtu na kugundua kuwa uwezo wake kitandani umebadilika ghafla kutokana na umri au mataizo mengine ya kiafya, unatakiwa kukubali tatizo na kumpa ushirikiano ili kuepusha matatizo.

Kilele na mwanamke:
Mwanamke anafika kileleni kuanzia Dk 10 mpaka dk 45 tangu tendo lianze na pengine inaweza kuchukua muda mrefu zaidi, hivyo basi kama unafanikiwa kufika kileleni ni wazi kuwa mumeo anauwezo wa kwenda mwendo wa angalau Dk15-20 sio dakika  3  kama  ulivyosema!

Napenda utambue kuwa uwezo wa tendo kwa wanawaume unatofautiana kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake, suala muhimu ni upendo mlionao (mnapendana) na yeye anauuwezo wa kulifanya tendo mpaka wote mnafikia mshindo nakuridhika.
Mawasiliano wakati wa Tendo:
Suala lingine hapa ni kutojua namna ya kucheza na wewe au mwili wako, kama unapenda kuchezewa zaidi kabla ya tendo la ndoa ni wajibu wako kuliweka hilo wazi na kumuelekeza mumeo wapi pa kushika, usitegemee yeye afanye hivyo kwani hajui nini unachokitaka au kukipenda. Ili ufurahie tendo na lifanywe your way unatakiwa kuwasiliana na mumeo wakati tendo linaendelea....


Kama nilivyosema hapo awali sio wanaume wote wanauwezo wa kufanya  mapenzi unaofanana, hivyo basi kama yeye anamudu asubuhi na jioni au asubuhi mchana na jioni (weekends) then kubali utaratibu huo kuliko kulazimisha afanye ulivyozoea wewe mara tatu katika saa moja.....ni ngumu kwa baadhi ya wanaume hasa wenye umri wa miaka 35 na zaidi.

Ni matumaini yangu utafanyia kazi ushauri kutoka kwa wachangiaji wengine na kuongezea maelezo ya hapo juu  ili kuishi maisha mazuri na yenye amani kwa faida yako, mumeo na watoto wenu

LAZIMA TUZIKAGUE KUCHA ZA LEMA..... TUPO TAYARI KUFA....."HAYA NI BAADHI YA MABANGO YA WAANDAMANAJI HUKO ARUSHA










































Asubuhi ya leo, kama ilivyotarajiwa na wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa mahakamani baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013.


Mbele ya hakimu Joyce Msofe na mawakili Kimomogoro na Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”
 

Mtuhumiwa Lema amekana kosa hilo.Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana.

Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja.

Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea kwenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA. kwa maandamano  makubwa


Picture

Picture Picture

Sunday 28 April 2013

SIONI TATIZO KWA LULU MICHAEL KUPIGA PICHA NA PENNY....HUO NI UMBEA WA MAGAZETI"..WEMA SEPETU

Hivi  karibuni  zilisambaa  picha  za  Lulu  Michael  akiwa  katika  picha  ya  pamoja  na  Penny....
Picha  hizo  zilizua  utata  mkubwa  miongoni  mwa  watu  huku  kundi  kubwa  likidai  kuwa  picha  hizo  zimepigwa  makusudi  kwa  lengo  la  kumuumiza  Wema  Sepetu...
Lulu Michael  akiwa  na Penny
Madai  hayo  yaliandikwa  kwa  kina  na  gazeti  moja  la  udaku  hapa  nchini  likisimulia  ugomvi   uliopo  kati  ya Penny  na Wema Sepetu.....
Waswahili  husema:
             Kama  A=B   na    B=C    basi   C= A  pia...!!!! 

Huo  ndo  ulikuwa  mtazamo  wa  gazeti  hilo  kusuhu  ukaribu  wa  Penny  na Lulu Michael.....

Akizijibu  tuhuma  hizo,Wema  Sepetu  ameamua  kuvunja  ukimya  na  kudai  kuwa  hawezi  kuwa  na  beef  na  baby  wake  Lulu  kwa  sababu  ya  Penny.....
Huu  ndo  ujumbe  wake

UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA


"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER

Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. 


Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
 
“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
 
Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
 
Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.

Source: Mwananchi

Wanaume huvutiwa kufanya mapenzi na rafiki za wake zao




Tafiti nyingi duniani zimegundua kuwapo na msukumo na mhemko wa tamaa za ngono kwa wanaume. Majibu kadha wa kadha ya tafiti hizo yamekuwa yakitoa majibu sawa, ikiwemo suala la maumbile ya mwanamume na namna anavyompokea mwanamke yoyote machoni pake.

Rafiki yangu wa karibu niliyempokea na kumtafutia kazi nchini Marekani alinisaliti kwa kutembea na mume wangu,” anaanza kwa kusema Christina Edward (34) (siyo jina lake kamili) Mtanzania anayeishi katika Jimbo la Houston Texas nchini Marekani. Christina anasema haikumuwia rahisi kung’amua tukio hilo la aibu, mpaka alipotonywa na jirani yake ambaye hakuwa na ukaribu naye. “Jirani yangu aliwaona, akanipa taarifa za usaliti huo. Nilifuatilia kwa muda mrefu na kuwakuta wakiwa katika flat (nyumba) anayoishi rafiki yangu huyo iliniuma sana, mpaka leo siweziRead more


Saturday 27 April 2013

DAYNA NYANGE AMPIGIA SALUTI AFANDE SELE

DAYNA NYANGE AMPIGIA SALUTI AFANDE SELE KWA TUNGO KALI


Mwanamuziki  toka  mkoani  Morogoro  anayefanya  poa  kwa  sasa  na  wimbo  wake  wa  Leo  mwanadada  Dayna  Nyange  a.k.a  Mkali  wao,  amefunguka  na  kumpigia  saluti mwanamuziki  mkongwe toka  hapa  Morogoro Afande  Sele.

Akiongea  na  mwandishi wetu   toka jijini Mwanza  aliko  sasa  katika  ziara  ya kimuziki  na  uzinduzi  wa  Albam  ya  Kala.  Dayna  amesema  huwa  anamkubali  afande kwa  tungo  zake

 '' kwa  kweli  siku  zote,  nimekuwa  nikimkubali  sana  Afande  sele  kwa  tungo  zake  zenye  ujumbe,  lakini  kwa  wimbo  huu wa  Dini tumeletewa,  nampigia  saluti.
 Afande  ni  bonge  la msanii  na  huwa naskiliza  nyimbo  zake kwani  najuwa  nikiskiliza  nyimbo  zake  kuna  madini  napata,  lakini  sasa kaka  mkubwa  kwa  hapa  alipofikia  na kufikilia  kwa  kina juu  ya  wimbo  huu,  anastahili  kuwa mfalme wa  Rhyme,  waliompa  tuzo  hawakukosea. 

Big  up  sana  Afande, saluti  kwake,  aendelee kuwa  mwalimu  wa  ujumbe  , huuwimbo  ni  zaidi  ya  Hotuba  ya  kitaifa Inayotolewa  na  Rais'' Amesema Dayna
 Ubalozini

DIAMOND-LONDON

"SIWAOGOPI MATAIRA WANAONIPONDA....MUNGU PEKEE ANAWEZA NA SI HAO TUMBIRI".....HII NI KAULI YA DIAMOND

Watu kadhaa  wamekuwa  wakimponda Diamond  baada ya  kwenda  LONDONI kwa  madai kuwa ni mshamba  wa  jiji  na  limbukeni ....

Madai hayo yamekuja  baada ya msanii huyu kuanza kuyashobokea  magari ya kifahari kwa kupiga nayo  picha na kuzirusha hewani.....

Baada ya kuona  mizengwe  ya watu imekuwa  mingi, Diamond  ameamua kuwajibu  kwa kupost  jumbe  huu

PAROKO- IFUNDA APOTEZA MAISHA KATIKA AJALI AKITOKA MSIBANI NJOMBE

PAROKO- IFUNDA APOTEZA MAISHA KATIKA AJALI AKITOKA MSIBANI NJOMBE


PAROKO  wa kanisa la RC parokia ya Ifunda Alphonce Mhamilawa amefariki  dunia katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea katika eneo la Sabasaba Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mashuhuda  wa  ajali  hiyo wameueleza mtandao  huu  kuwa ajali  hiyo ilitokea  majira ya saa 2 usiku  wa  kuamkia  leo wakati paroko  huyu akitoka mkoani Njombe katika  shughuli  ya Mazishi

Mmoja kati ya mashuhuda  hao Bw  Saugo Ndemo  alisema  kuwa paroko  huyo alikuwa akiendesha gari dogo aina ya Toyota  Hilux (Pick Up) yenye  namba  za usajili  T434 APP mali ya Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo  alisema  kuwa chanzo  cha ajali  hiyo ni Paroko  kuligonga gari aina ya Lori  kwa  nyuma na kuwa lori  hilo halikuweza  kusimama.

Alisema  kuwa  paroko  huyo alifia eneo la tukio baada ya  ajali  hiyo  iliyopelekea  kichwa  chake  kupasuka.

Mmoja kati ya askari  wa usalama barabarani ambae hakutaka  kutaja jina lake kwa  kuwa si msemaji  mkuu  wa  jeshi la  polisi alisema  kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi.

Pia alisema kuwa lori ambalo paroko huyo aliligonga linasadikika  kuwa lilibeba mbao huku  likivutana na  lori  jingine na baada ya ajali  hiyo halikuweza  kusimama.

ARIS UDOM

Open ARIS-UDOM here...

UDOM SR


Open UDOM-SR here...


WACHUMBA

NATAFUTA MCHUMBA MWAMINIFU

Mary
mary ndo jina langu natokea kahama,na nina diploma, natafuta mchumba awe mkristo,mrefu, mweupe,asivute wala kunywa pombe,awe na kazi na elimu angalua
chuo kikuu,wacliana na mm kwa no.0758051743

......

mimi ni msichana mjasiri mali na pia msomi.mimi naishi arusha, ila kwa sasa nipo dar es salaam kwani ninasoma,napenda kuwa na rafiki ambaye ni msomi na
mcheshi msafi na mtafutaji.kiufupi mimi ni mchagga kwangu kabila si chagui namba zangu za simu ni 0766635368

------
 naitwa brian malembeka nipo dodoma natafuta mchumba wa kike alie serious na maisha anejua thamn ya kupendwa tutaependana nae ktk shida na raha anaejieshim mtaratibu mstaarabu alie tayar kupima sitafuti mchumba ku jishow off nahitaj wa kuwa nae maishan alie serious 0718546050 usibip sipend kubipiwa
-----

LEMA KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU


GODBLESS LEMA KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU



MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau. 

 "Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.

Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo.

Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.

Mbune huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.



AMALI JIJINI ARUSHA

SAM_0651Pichani ni wafanyakazi wa kampuni Afrikan Barrik wakiwaonyesha wananchi jinsi ya okoaji wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi migodini kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha kwa siku Tatu yakiwa ni mwengelezo wa warsha ya mamlaka ya usalama mahala pa kazi(OSHA)  SAM_0661 SAM_0669 SAM_0672 SAM_0676Banda la wauzaji wa dawa kutoka china kampuni ya TIENS ambao nao walishiriki katika maonyesho yaliondaliwa na mamlaka ya usalama mahala pa kazi OSHA wakionyesha bidhaa wanazouza kwenye maonyesho hayo huku wakiwataka wananchi wafike ofisini kwao jengo la KKKT jijini hapa kupata bidhaa zao na pichani ni muuzaji wa dawa hizo bi Beatrice Kiimbi kama alivyokutwa na kamera yetu kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha. George Alando meneja usalama na afya wa kampuni ya Layne Driling ya jijini Morogoro akiwa na mwenzake kwenye banda lao wakati wa maonyesho ya usalama mahala pa kazi yanayoendelea jijini Arusha na yatafunguliwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda siku ya jumapili ambayo itakuwa ni siku ya ukoaji mahala pa kazi SAM_0680
SAM_0678
George Alando meneja usalama na afya wa kampuni ya Layne Driling ya jijini Morogoro akiwa na mwenzake kwenye banda lao wakati wa maonyesho ya usalama mahala pa kazi yanayoendelea jijini Arusha na yatafunguliwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda siku ya jumapili ambayo itakuwa ni siku ya ukoaji mahala pa kazi. Picha zotE na Mahamoud Ahmad Arusha