Friday 3 May 2013

Mfanyabiashara kariakoo ajirusha toka Ghorofa ya tisa na kuangukia Gari

b1[1]
Mtu huyo amekimbizwa hospitali na haijafahamika bado kama amefariki au bado yu hai.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo. Chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita, wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.

No comments:

Post a Comment