Lulu aliwakia gazeti la udaku kwa habari za uongo
Baada ya Batuli, Lulu naye aliwakia gazeti moja la udaku kwa habari za uongo! Soma zaidi...

Katika kile kinachoonekana kukerwa na vitendo vya vyombo vingi
vya habari hususani magazeti ya kadhaa ya udaku yanoyochapisha habari za
uongo kuhusu wasanii wa bongo movies kwa ajili ya kuuza magazeti yao,
hatimaye msanii Elizabeth Michael “lulu”naye ameamua kuyaweka wazi ya
moyoni mwake bila kuficha baada ya gazeti moja pendwa (Jina
tunalihifadhi) kuchapisha habari iliyopew kichwa kisemacho “Lulu, wema,
Diamond afya mgogoro”ambayo imeonekana dhahiri kumkera mrembo huyu na
kuamua kaundika haya yafuatayo kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa
kijamii.
“..Imekuwa ni kawaida ya mtu kujisikia kusema
chochote...muda mwingine mnaweza mkahisi hatuoni au mkahisi kukaa kwetu
kimya ni wajinga!!mm kama mm napenda kuwajulisha kuwa LULU mliyekuwa
mnamjua sio LULU wa ss...msitegemee kusikia nabisha au kupigizana
kelele...fanyeni kazi yenu lakini sio kuchafuana na kuipotosha
jamii....!!!nadhani kimya changu kina majibu mengi..
Lulu anakuwa msanii wa pili kwa kipindi cha wiki mbili
kukasirika hadharani baada ya mwanadada batuli kulaani kitendo cha
gazeti moja la udaku kuandika habari za uongo kuhusu yeye.
No comments:
Post a Comment